Jun 14, 2021

SULEIMAN SHAHBAL AHAMA JUBILEE NA KUTANGAZA AZMA YAKE.

Aliyekuwa Mwaniaji wa Kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal amekihama chama cha Jubilee na kuregea katika chama Cha ODM huku uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ukikaribia. 

Hatua yake hiyo inakuja chini ya mwongo mmoja tangu alikipokigura chama hicho , baada ya kupoteza kura za mchujo kwa gavana Ali Hassan Joho. 

Kupitia kwa mkanda wa video aliyouweka katika ukurasa wake wa Facebook hapo jana, Shahbal ambaye alikuwa akilihutubia kundi la jamii ya waluo kaunti ya Mombasa(MLFG) alionyesha azma yake ya kumrithi Gavana Ali Hassan Joho ambaye uongozi wa mihula yake miwili unatamatika baada ya miezi 13 ijayo. 

Aidha katika hotuba yake, Shahbal alimpigia debe kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na kusema kuwa ni kiongozi ambaye ameipigania nchi hii kwa ajili ya demokrasia hivyo basi ni wakati muafaka kwake kuliongoza taifa hili. 
Vile vile mfanyibiashara huyo alihimiza umoja katika ya Raila na Kalonzo,  na kusema kuwa itakuwa furaha kubwa kuona viongozi hao wawili wakishika usukani wa kuliongoza taifa hili. 

Jun 12, 2021

RAILA AITAKA SERIKALI KUTOA SABABU ZA KUWATEMA MAJAJI SITA

 Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga, Ameitaka serikali kuweka wazi maswala  yaliyopelekea kutoteuliwa majaji Sita kati ya arubaini waliyopendekezwa kwa uteuzi na tume ya huduma za Mahakama JSC. 
Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya jumamosi , kiongozi huyo wa ODM amewarai rais, maspika wa bunge la kitaifa na seneti pamoja na jaji mkuu kuweka nguvi zao pamoja haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuendesha serikali kikamilifu.
 
Wakati huo huo ametoa changamoto kwa serikali kutoa ushahidi wake uliyopelekea kutemwa kwa majaji sita, kwa idara ya mahakama na wakenya kwa ujumla.Amesema kenya haiwezi kuhimili vita baina ya taasisi za serikali. 

Aidha Raila, Amesema kuwa tangu kenya ilipojipatia katiba mpya ya sasa, nguzo tatu kuu za serikali zimekuwa zikijihusisha na malumbano na athari yake taifa limeshuhudia migorogoro ya kitaifa. 

Jun 11, 2021

WAZIRI YATANI AAINISHA SERA SABA ZA KUFUFUA UCHUMI.


Waziri wa hazina ya kitaifa Ukur Yatani amebainisha sera saba zilizopewa kipaumbele na serikali kwa ajili ya kufufua uchumi wa nchi kwa kasi kutokana na athari zilizoletwa na janga la Covid19.
 Akisoma taarifa ya bajeti ya mwaka 2021/2022,  Waziri Yatani alibainisha kuwa utekelezaji wa ajenda nne kuu za rais uhuru Kenyatta bado unabakia nyenzo muhimu ya kuufufua uchumi. 

Kutokana hilo, Waziri yatani amesema kuwa serikali itahakisha mipango na miradi chini ya ajenda nne kuu imewezeshwa. Miongoni mwazo ikiwa,  usalama wa chakula na lishe, Afya bora kwa wote, makaazi ya bei nafuu na ukuaji wa sekta ya viwanda/uzalishaji kwa ajiili ya kupunguza ukosefu wa ajira. 

Kufikia lengo hili ,waziri alidokeza kuwa serikali itachukua hatua za kimkakati zitakazo nuia kuhakikisha maendeleo endelevu ya kiuchumi Miongoni mwa hoja nyingine. 

Jun 9, 2021

WABUNGE WATISHIA KUTATIZA USOMWAJI WA BAJETI ALHAMISI

Wabunge wa bunge la kitaifa wanatishia kulemaza vikao vya bunge siku ya alhamisi wakati wa usomwaji wa bajeti ya kitaifa,  kwa kile wanachodai ni uchekeshwaji wa usambazaji kwa pesa za ustawishaji wa maeneo bunge CDF. 

Awali Mwezi machi mwaka huu waziri wa hazina ya kitaifa ukur yattani aliahidi kutoa shilingi bilioni 2 kila wiki hadi mwisho wa mwaka wa kifedha 2020/2021.
Kulingana na wabunge ahadi bado  hiyo haijatimizwa. 

 Mwezi huo wa Machi aidha wabunge Waliikosoa hazina ya kitaifa wakiapa kuiangusha miswada ya serikali inayohusu hazina hiyo kama ingeshindwa kusambaza pesa hizo.

Hatahivyo ilibainika kuwa maeneo bunge 290 tayari yamepokea kiwango cha shilingi milioni 20 pekee kati ya milioni 137 kwa mwaka huu wa kifedha. 

Jun 8, 2021

VIONGOZI WATAKA SERIKALI IFUFUE MIRADI BONDE LA UFA

Viongozi kutoka mrengo unaomuegemea naibu wa rais William Ruto wanamtaka rais Uhuru Kenyatta kuhakikisha miradi yote iliyosimamishwa katika ngome ya Naibu wake inafufuliwa. 

Kundi hilo likiongozwa na gavana wa Turkana Josephat Nanok limesema kuwa limeridhishwa na miradi ya rais uhuru katika maeneo mbalimbali nchini na sasa wanaitaka miradi iliyosimama katika eneo la bonde la ufa pia iendelezwe. 

Wakihutibia wanahabari baada ya mkutano wa majadiliano ya pamoja na viongozi kutoka eneo la bonde la ufa, viongozi hao wamesema kuwa miradi ya mabwawa mbalimbali iliyoanzishwa na serikali inapaswa kumalizwa kwa faida ya wananchi katika eneo hilo. 


Mbali na miradi iliyokwama, viongozi hao wanaojumuisha magavana,  maseneta, wabunge na wawakilishi wadi, vilevile waliweka wazi kuwa yapo mambo muhimu yanayohusu eneo hilo ambayo yatatakiwa kuongelewa na serikali itakayoundwa baada ya uchaguzi unaokuja. 

Jun 7, 2021

WATU KUMI WAKAMATWA NDANI YA KLABU YA USIKU WAKIJIVINJARI.

Polisi katika eneo bunge la Kuria Magharibi kaunti ya Migori wanawazuilia watu kumi waliyopatikana wakijivinjari katika klabu cha usiku,  usiku wa jumapili. 

Miongoni mwa waliokamatwa wakati wa msako huo ni mhudumu wa klabu hiyo, Michael Chacha Marwa, mwenye umri wa miaka 20 ambaye atakabiliwa na mashtaka ya kuendesha operasheni ya klabu hicho cha usiku bila ya kibali na pia kupuuzilia mbali sheria za Covid19 za uuzaji wa pombe. 

Kamanda wa polisi eneo la Kuria Magharibi Cleti Kimaiyo,  amesema kuwa watuhumiwa tisa waliyokamatwa watashtakiwa kwa kosa la kupuuza amri ya kafyu iliyowekwa na serikali. 

Aidha amesema kuwa mmiliki wa kablu hiyo johness Mwita alifanikiwa kutoroka na wako katika harakati za kumkamata. 
Vile vile aliongeza kuwa msako huo utaendelezwa, na kutoa onyo kwa watu wanaopuuzilia sheria za Covid19 zilizowekwa kuwa chao kimotoni. 


Jun 5, 2021

MAAFISA WA MAGEREZA WAKAMATWA KWA KUHUSISHWA NA KAZI GHUSHI.

 Polisi wamewakamata washukiwa watatu zaidi wanaohusishwa na sakata ya utoaji kazi ghushi iliyogunduliwa na Makachero wa idara ya DCI wiki mbili zilizopita.
Kulingana na mkurugenzi wa DCI George Kinoti, mamia ya watu wanaotafuta kazi wanaaminika kupoteza zaidi ya milioni 200 katika ulaghai huo, baada ya kuahidiwa kazi katika mashirika mbalimbali ya serikali,  ikijumuisha vitengo muhimu vya kiusalama vya serikali.
 
Washukiwa wawili walikamatwa siku ya ijumaa. Senior Sergent Jackson Mureithi Manyara na corporal Zachary Kimathi Cosmas, ni maafisa wa magereza Wanaoaminika kuwa walisajiliwa na mshukiwa  mkuu Grace Nyamohanga, jukumu lao likiwa kupokea pesa kwa ajili ya kazi hizo hewa. 

Mshukiwa wa tatu Peter Ngare Githu, ambaye makaazi yake yako eneo la juja kaunti ya Nairobi,  anaamika kusajili watu 50 na kukusanya milioni 16 kutoka kwao. 

Watatu hao wanatarajiwa kuwasilishwa mahakamani siku ya jumatatu pamoja na Grace Nyamohanga na Masiaga Slvester, kwa ajili ya kusomewa mashtaka. 





Jun 4, 2021

VYAMA VYA KMJA NA LSK VYAMKOSOA RAIS UHURU KUHUSIANA NA UTEUZI WA MAJAJI.

Chama cha Mahakimu na majaji nchini (KMJA) na kile cha wanasheria (LSK) Kwa pamoja vimemkosoa rais Uhuru Kenyatta kwa kile wanachodai ni uteuzi wa majaji kibaguzi.
Haya yanajiri siku moja tu baada ya rais Uhuru Kenyatta kuwateuwa majaji waliyopendekezwa na tume ya huduma za mahakama (JSC) zaidi ya miaka miwili iliyopita. Hata hivyo cha kushangaza rais uhuru aliteuwa majaji 34 pekee na kukataa uteuzi wa majaji sita.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari chama cha KMJA kimesema kuwa rais uhuru Kenyatta anawajibishwa kisheria Kuwateuwa majaji wote waliyopendekezwa na tume ya JSC. 
Katibu mkuu wa chama cha KMJA amesema kuwa majina yanapopendekezwa na JSC kwa ajili ya uteuzi , rais hana wajibu wowote kisheria kufanya mabidiliko, kwani kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa tume hiyo
 
Aidha chama cha LSK kwa upande wake kimeongezea  kuwa kitendo cha rais kushindwa kuteua majaji ndani ya siku 14 zilizoweka baada ya kupendekezwa  na tume ya JSC ni ukiukaji wa sheria. 

Jun 3, 2021

POLISI WANASA BUNDUKI NANE HARAMU NA RISASI KWA MWENZAO

Maafisa kutoka idara ya upelelezi DCI na wenzao kutoka idara ya polisi kituo cha Cherangani,  mnamo usiku wa jumanne walifanikiwa kupata bunduki nane kwa pamoja katika nyumba ya afisa wa polisi anayehudumu Nairobi. 

Kulingana na polisi kutoka kituo cha Cheranganyi, nyumba waliyoivamia ina milikiwa na Maxwell Tally Mutonyi ambaye ni afisa wa polisi dereva anayehudumu katika idara ya mahakama lakini anaishi katika makaazi ya maafisa wa polisi yaliyoko South B jijini Nairobi. Polisi wanasema kuwa alitoweka muda mfupi baada ya wao kuvamia nyumba yake.

Wakati wa msako huo maafisa wa polisi walifanikiwa kupata bunduki aina ya UZI SMG ikiwa na risasi S/No.  09234, smith na Wesson revolver S/No.38SPL, Six Germany Walther pistols S/Nos BE5768, XB3026, BP4957, AW5339, ME8395 na HJ6205  magazines, 197.pamoja na risasi nyengine. 
Afisa huyo wa polisi anatarajiwa kukamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Jun 1, 2021

VIONGOZI WATAKA UJENZI WA BANDARI YA SAMAKI YA SHIMONI UENDELEZWE

Serikali imehimizwa kuutafakari upya na kuufufua ujenzi wa bandari  ya samaki uliyosimama katika eneo la Shimoni kaunti ya Kwale. 

Viongozi kutoka ukanda wa pwani wanaitaka serikali ya kutaifa kuja na ari mpya na kuukamilisha ukarabati wa bandari hiyo ambayo wanasema itapiga jeki na kuinua sekta ya uvuvi eneo hilo.
 
Ujenzi wa bandari hiyo ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kitaifa kuendeleza na kupanua uchumi wa baharini. 
Bandari hiyo aidha inatarajiwa kuwa na athari chanya katika sekta ya biashara na ukuaji wa uchumi kiujumla. 

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...