Polisi katika eneo bunge la Kuria Magharibi kaunti ya Migori wanawazuilia watu kumi waliyopatikana wakijivinjari katika klabu cha usiku, usiku wa jumapili.
Miongoni mwa waliokamatwa wakati wa msako huo ni mhudumu wa klabu hiyo, Michael Chacha Marwa, mwenye umri wa miaka 20 ambaye atakabiliwa na mashtaka ya kuendesha operasheni ya klabu hicho cha usiku bila ya kibali na pia kupuuzilia mbali sheria za Covid19 za uuzaji wa pombe.
Kamanda wa polisi eneo la Kuria Magharibi Cleti Kimaiyo, amesema kuwa watuhumiwa tisa waliyokamatwa watashtakiwa kwa kosa la kupuuza amri ya kafyu iliyowekwa na serikali.
Aidha amesema kuwa mmiliki wa kablu hiyo johness Mwita alifanikiwa kutoroka na wako katika harakati za kumkamata.
Vile vile aliongeza kuwa msako huo utaendelezwa, na kutoa onyo kwa watu wanaopuuzilia sheria za Covid19 zilizowekwa kuwa chao kimotoni.