Kinara wa Chama cha ODM Raila Odinga, Ameitaka serikali kuweka wazi maswala yaliyopelekea kutoteuliwa majaji Sita kati ya arubaini waliyopendekezwa kwa uteuzi na tume ya huduma za Mahakama JSC.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari siku ya jumamosi , kiongozi huyo wa ODM amewarai rais, maspika wa bunge la kitaifa na seneti pamoja na jaji mkuu kuweka nguvi zao pamoja haraka iwezekanavyo kwa ajili ya kuendesha serikali kikamilifu.
Wakati huo huo ametoa changamoto kwa serikali kutoa ushahidi wake uliyopelekea kutemwa kwa majaji sita, kwa idara ya mahakama na wakenya kwa ujumla.Amesema kenya haiwezi kuhimili vita baina ya taasisi za serikali.
Aidha Raila, Amesema kuwa tangu kenya ilipojipatia katiba mpya ya sasa, nguzo tatu kuu za serikali zimekuwa zikijihusisha na malumbano na athari yake taifa limeshuhudia migorogoro ya kitaifa.