Jun 24, 2023

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa


Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai na wale wa Mbunge wa Nyali Mohammed Ali  kuonyeshana ubabe wa kisiasa.

Kizazaa kilizuka  pale mbunge wa Nyali Mohamed Ali aliposhambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa  wafuasi wa  Hassan Omar Sarai  wakati alipowasili kwenye ukumbi wa mkutano huo, Hali iliyopekelea   kurushwa kwa vitoza machozi  na watu  wasiojukikana ili kuutawanya umati uliyokuwa umejaa ukumbini humo.



Matukio hayo yalilazimu kuhairishwa kwa mkutano huo wa wajumbe  ambao ulikuwa umeandakiwa kwa lengo la kuwahamasisha wanachama wa UDA kuhusiana na uchaguzi wa chama hicho  unaotarajiwa kuandaliwa mnamo Mwezi Agosti pamoja na kujadiliwa kwa ajenda za chama.



Hatahivyo akihutubia  wanahabari kuhusiana na matukio hayo Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amemkosoa Hassan Omra sarai kwa madai ya kutumia vibaya nafasi yake kwenye chama UDA   ili kuhujumu matokea ya uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa  Mwezi Agosti.

Mbunge huyo  amemtaka Sarai kujikita katika majukumu yake kama Mbunge wa Kenya kwenye bunge la Afrika Mashariki badala ya kujihusisha na siasa za chama hicho  na kuleta migawanyiko.

Kwa upande wake Hassan Omar Sarai amemtuhumu mbunge huyo wa  Nyali kwa madai ya kughushi kadi za wajumbe waliyoalikwa kuhudhuria mkutano huo akidai  kuwa wengi wafuasi wake hakuwa  wajumbe halisi  wa UDA bali watu waliyokuwa na nia ya kuzua ghasia kwenye mkutano huo.

Wakati huo huo Sarai amepuuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na mbunge hiyo yakumtuhumu kuwa na nia ya  kuhujumu uchaguzi wa chama hicho huku akibainisha kama naibu mwenyekiti wa chama hicho hana nia ya kufanya hivyo.

 Amekashifu ghasia zilizishuhudiwa wakati wa mkutano huo  huku akipuuzilia mbali madai kuwa analenga kuhujumu uchaguzi wa chama hicho.

Naye katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala ambaye alikuwa amehudhuria mkutano amesisitiza Kuwa uongozi wa  chama hicho kamwe hautaegemea upande wowote katika uchaguzi unaokuja huku akiwataka viongozi hao wawili kukaa chini na kuzika tofauti zao.

Wakati huo huo amesema kuwa chama kitalazimika kuchukua hatua za kinidhamu kwa kiongozi yeyote atakayepatikana kuhisika na ghasia zilizishuhudiwa wakati wa mkutano huo.

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...