Aliyekuwa Mwaniaji wa Kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal amekihama chama cha Jubilee na kuregea katika chama Cha ODM huku uchaguzi mkuu wa mwaka 2022 ukikaribia.
Hatua yake hiyo inakuja chini ya mwongo mmoja tangu alikipokigura chama hicho , baada ya kupoteza kura za mchujo kwa gavana Ali Hassan Joho.
Kupitia kwa mkanda wa video aliyouweka katika ukurasa wake wa Facebook hapo jana, Shahbal ambaye alikuwa akilihutubia kundi la jamii ya waluo kaunti ya Mombasa(MLFG) alionyesha azma yake ya kumrithi Gavana Ali Hassan Joho ambaye uongozi wa mihula yake miwili unatamatika baada ya miezi 13 ijayo.
Aidha katika hotuba yake, Shahbal alimpigia debe kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na kusema kuwa ni kiongozi ambaye ameipigania nchi hii kwa ajili ya demokrasia hivyo basi ni wakati muafaka kwake kuliongoza taifa hili.
Vile vile mfanyibiashara huyo alihimiza umoja katika ya Raila na Kalonzo, na kusema kuwa itakuwa furaha kubwa kuona viongozi hao wawili wakishika usukani wa kuliongoza taifa hili.