
NA NYOTA SULEIMAN MOHAMED
Viongozi mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kuwahimiza wananchi kujiandikisha kama wapiga kura kabla la zoezi kufungwa.
katika kaunti ya Mombasa Uongozi wa chama cha ODM umefanya misururu ya mikutano katika eneo bunge la Changamwe ili kuwahamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kujisajili kama wapiga kura pamoja kujiandikisha kuwa wanachama wa chama hicho.
Akiongoza msafara huo Mwenyekiti wa Chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohamed Khamid Khamis maarufu DEE amewarai wananchi katika eneo bunge hilo kujisajili kwa wingi kama wapiga kura ili kumpeleka Ikulu kinara wa Chama hicho Raila Odinga baada ya uchaguzi mkuu.
Aidha Mohamed ameendelea kusisitiza kuwa uteuzi wa chama hicho utafanyika kwa njia huru na haki,akiwahimiza wakaazi wa Changamwe kuchukua kura kwa wingi na kusajili katika chama cha ODM , akisema kuwa ni wale waliojisajili na chama pekee ndio watakao ruhusiwa kupiga kura katika kura za mchujo.
Kwa Upande wake katibu mkuu wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Geoffrey Busaka ameendelea kumpigia debe kinara wa chama hicho Raila Odinga akisema kwamba juhudi za kinara wa chama cha ODM Raila Odinga za kuingia ikulu zitategemea mno na kura za Wakaazi wa Kaunti nzima ya Mombasa.
