Waziri wa hazina ya kitaifa Ukur Yatani amebainisha sera saba zilizopewa kipaumbele na serikali kwa ajili ya kufufua uchumi wa nchi kwa kasi kutokana na athari zilizoletwa na janga la Covid19.
Akisoma taarifa ya bajeti ya mwaka 2021/2022, Waziri Yatani alibainisha kuwa utekelezaji wa ajenda nne kuu za rais uhuru Kenyatta bado unabakia nyenzo muhimu ya kuufufua uchumi.
Kutokana hilo, Waziri yatani amesema kuwa serikali itahakisha mipango na miradi chini ya ajenda nne kuu imewezeshwa. Miongoni mwazo ikiwa, usalama wa chakula na lishe, Afya bora kwa wote, makaazi ya bei nafuu na ukuaji wa sekta ya viwanda/uzalishaji kwa ajiili ya kupunguza ukosefu wa ajira.