Serikali imehimizwa kuutafakari upya na kuufufua ujenzi wa bandari ya samaki uliyosimama katika eneo la Shimoni kaunti ya Kwale.
Viongozi kutoka ukanda wa pwani wanaitaka serikali ya kutaifa kuja na ari mpya na kuukamilisha ukarabati wa bandari hiyo ambayo wanasema itapiga jeki na kuinua sekta ya uvuvi eneo hilo.
Ujenzi wa bandari hiyo ni sehemu ya mikakati ya serikali ya kitaifa kuendeleza na kupanua uchumi wa baharini.
Bandari hiyo aidha inatarajiwa kuwa na athari chanya katika sekta ya biashara na ukuaji wa uchumi kiujumla.