Jun 24, 2023

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa


Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai na wale wa Mbunge wa Nyali Mohammed Ali  kuonyeshana ubabe wa kisiasa.

Kizazaa kilizuka  pale mbunge wa Nyali Mohamed Ali aliposhambuliwa na watu wanaodaiwa kuwa  wafuasi wa  Hassan Omar Sarai  wakati alipowasili kwenye ukumbi wa mkutano huo, Hali iliyopekelea   kurushwa kwa vitoza machozi  na watu  wasiojukikana ili kuutawanya umati uliyokuwa umejaa ukumbini humo.



Matukio hayo yalilazimu kuhairishwa kwa mkutano huo wa wajumbe  ambao ulikuwa umeandakiwa kwa lengo la kuwahamasisha wanachama wa UDA kuhusiana na uchaguzi wa chama hicho  unaotarajiwa kuandaliwa mnamo Mwezi Agosti pamoja na kujadiliwa kwa ajenda za chama.



Hatahivyo akihutubia  wanahabari kuhusiana na matukio hayo Mbunge wa Nyali Mohammed Ali amemkosoa Hassan Omra sarai kwa madai ya kutumia vibaya nafasi yake kwenye chama UDA   ili kuhujumu matokea ya uchaguzi unaotarajiwa kuandaliwa  Mwezi Agosti.

Mbunge huyo  amemtaka Sarai kujikita katika majukumu yake kama Mbunge wa Kenya kwenye bunge la Afrika Mashariki badala ya kujihusisha na siasa za chama hicho  na kuleta migawanyiko.

Kwa upande wake Hassan Omar Sarai amemtuhumu mbunge huyo wa  Nyali kwa madai ya kughushi kadi za wajumbe waliyoalikwa kuhudhuria mkutano huo akidai  kuwa wengi wafuasi wake hakuwa  wajumbe halisi  wa UDA bali watu waliyokuwa na nia ya kuzua ghasia kwenye mkutano huo.

Wakati huo huo Sarai amepuuzilia mbali madai yaliyoibuliwa na mbunge hiyo yakumtuhumu kuwa na nia ya  kuhujumu uchaguzi wa chama hicho huku akibainisha kama naibu mwenyekiti wa chama hicho hana nia ya kufanya hivyo.

 Amekashifu ghasia zilizishuhudiwa wakati wa mkutano huo  huku akipuuzilia mbali madai kuwa analenga kuhujumu uchaguzi wa chama hicho.

Naye katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala ambaye alikuwa amehudhuria mkutano amesisitiza Kuwa uongozi wa  chama hicho kamwe hautaegemea upande wowote katika uchaguzi unaokuja huku akiwataka viongozi hao wawili kukaa chini na kuzika tofauti zao.

Wakati huo huo amesema kuwa chama kitalazimika kuchukua hatua za kinidhamu kwa kiongozi yeyote atakayepatikana kuhisika na ghasia zilizishuhudiwa wakati wa mkutano huo.

AFUENI KWA MADEREVA WA TUK TUK MOMBASA

 Na Nyota Suleiman




MADEREVA wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kampuni ya Car General Kuzindua rasmi aina mpya za Tuk Tuk PIAGGIO NXT zenye Muundo wa kipee ambazo zinatarajiwa kupiga Jeki biashara hiyo na kuiboresha zaidi katika kaunti hiyo.

Uzinduzi wa aina hiyo mpya ya Tuk Tuk  unajiri kufuatia malalamiko kutoka kwa madereva wa Tuk Tuk kuhusiana na mapungufu yaliyoshuhudiwa katika Tuk Tuk za  hapo awali zilizonunuliwa kutoka kwa kampuni hiyo.

Kulingana na raisi wa Muunganao wa madereva wa Tuk Tuk kaunti ya Mombasa ambaye pia ni mwanzilishi wa biashara hiyo katika kaunti  hiyo Chrispine Obondo maarufu Mr Dubai ameutaja uzinduzi huo kama hatua muhimu katika sekta ya uchukuzi katika kaunti ya Mombasa akisema itawasaidia pakubwa madereva wa Tuk Tuk  kumudu gharama ya biashara hususan bei ya mafuta kutokana na muundo  wa Kipekee wa Tuk Tuk Hizo.

Wakati huo huo ameipongeza kampuni ya Car and general kwa kutoa kipaumbele katika kuangazia maslahi na matatizo yanayowakumba Madereva na kutafuta suluhu muafaka ili Kuwawezesha kuendeleza biashara bila madhila yoyote.

Aidha  ametoa wito kwa madereva wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa kupewa mafunzo ya Kutosha kuwawezesha kuendeleza shughuli zao ipasavyo ili  kuwaepushia mahangaiko wanayopitia kutoka kwa maafisa trafiki katika kaunti hiyo.

Wakati huo huo ameonyesha kusikitishwa kwake na jinsi baadhi ya maafisa hao wa trafiki wamekuwa wakiwahanagaisha madereva wa tuk tuk bila  hatia ,akiwataka kukomesha hujuma dhidi yao.

Baadhi ya Madereva waliyozungumza katika hafla ya Uzinduzi huo iliyoandaliwa katika uga wa Makadara mjini Mombasa Wameonyesha furaha yao kutokana ujio wa Tuk Tuk hizo mpya huku wakiwarai wenzao kujiunga na miungano ya madereva ili wawaze kujinufaisha zaidi.

Kwa upande wao maafisa kutoka kampuni ya Car and general   waliyohudhuria uzinduzi huo wamewahimiza madereva kujitokeza na kuchukua mikopo ya kununua Tuk Tuk hizo mpya ili waweze kujiendeleza zaidi kichumi.


Nov 24, 2022

AFUENI KWA MADEREVA WA TUK TUK MOMBASA

Na Nyota Suleiman


Madereva wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kampuni ya Car General Kuzindua rasmi aina mpya za Tuk Tuk PIAGGIO NXT zenye Muundo wa kipee ambazo zinatarajiwa kupiga Jeki biashara hiyo na kuiboresha zaidi katika kaunti hiyo.

Uzinduzi wa aina hiyo mpya ya Tuk Tuk  unajiri kufuatia malalamiko kutoka kwa madereva wa Tuk Tuk kuhusiana na mapungufu yaliyoshuhudiwa katika Tuk Tuk za  hapo awali zilizonunuliwa kutoka kwa kampuni hiyo.

Kulingana na raisi wa Muunganao wa madereva wa Tuk Tuk kaunti ya Mombasa ambaye pia ni mwanzilishi wa biashara hiyo katika kaunti  hiyo Chrispine Obondo maarufu Mr Dubai ameutaja uzinduzi huo kama hatua muhimu katika sekta ya uchukuzi katika kaunti ya Mombasa akisema itawasaidia pakubwa madereva wa Tuk Tuk  kumudu gharama ya biashara hususan bei ya mafuta kutokana na muundo  wa Kipekee wa Tuk Tuk Hizo.

Wakati huo huo ameipongeza kampuni ya Car and general kwa kutoa kipaumbele katika kuangazia maslahi na matatizo yanayowakumba Madereva na kutafuta suluhu muafaka ili Kuwawezesha kuendeleza biashara bila madhila yoyote.

Aidha  ametoa wito kwa madereva wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa kupewa mafunzo ya Kutosha kuwawezesha kuendeleza shughuli zao ipasavyo ili  kuwaepushia mahangaiko wanayopitia kutoka kwa maafisa trafiki katika kaunti hiyo.

Wakati huo huo ameonyesha kusikitishwa kwake na jinsi baadhi ya maafisa hao wa trafiki wamekuwa wakiwahanagaisha madereva wa tuk tuk bila  hatia ,akiwataka kukomesha hujuma dhidi yao.

Baadhi ya Madereva waliyozungumza katika hafla ya Uzinduzi huo iliyoandaliwa katika uga wa Makadara mjini Mombasa Wameonyesha furaha yao kutokana ujio wa Tuk Tuk hizo mpya huku wakiwarai wenzao kujiunga na miungano ya madereva ili wawaze kujinufaisha zaidi.

Kwa upande wao maafisa kutoka kampuni ya Car and general   waliyohudhuria uzinduzi huo wamewahimiza madereva kujitokeza na kuchukua mikopo ya kununua Tuk Tuk hizo mpya ili waweze kujiendeleza zaidi kichumi.


Sep 15, 2022

ABDULSWAMAD AAPISHWA KUWA GAVANA MOMBASA


 Hatimaye aliyekuwa mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir ameapishwa rasmi kuwa gavana mpya wa kaunti ya Mombasa katika sherehe aliyoandaliwa katika bustani ya Mama Ngina Water Front Mjini Mombasa.

Abdulswamad ambaye anachukua hatamu ya kuwa gavana wa pili wa kaunti hiyo kutoka kwa aliyekuwa gavana Ali Hassan Joho,amewashukuru wakaazi wa kaunti ya Mombasa kwa kumpa nafasi ya kuongoza kaunti hiyo huku akiahidi kuwahudumia  wote bila ya kuwabagua.

Wakati huo huo Nassir amewarai waliyokuwa  wapinzani wake wa kisiasa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kiti hicho kuzika tofauti zao za kisiasa kuungana naye katika safari ya kuiendeleza na kuibadilisha  kaunti ya Mombasa kimaendeleo.

Hatahivyo akiwahutubia mamia ya wakaazi walijitokeza kushuhudia sherehe ya  kuapishwa kwake, Nassir ameahidi kuwa uongozi wake  utafanikisha Ugatuzi ipasavyo kwenye kaunti hiyo ili kuleta mageuzi ya kiuchumi na kutengeneza fursa za ajira kwa wakaazi.

Aidha Nassir amesema kuwa ndani ya siku mia moja za utawala wake atahakikisha kuwa huduma za serikali ya kaunti ya Mombasa zitapatikana kwa njia raisi kupitia mpango Huduma Mtaani ambao utabadilisha mchakato mzima wa kutafuta huduma kwenye kaunti hiyo.

Katika sekta ya afya  Abdulswamad amebainisha  kuwa serikali yake itaanzisha mpango wa afya care unaonuia kuwawezesha wakaazi kutoka familia maskini kwenye kaunti hiyo kupata huduma za matibabu wakati wanapokuwa wagonjwa.

wakati huo huo akisema kuwa  watatoa nafasi za mafunzo kwa madaktari ilikuwawezsha kutoa huduma za kiwango cha juu.

Vile Vile Katika Sekta ya elimu amesema kuwa serikali yake  itaweka mpango wa basari utakaowawezesha wanafunzi kusoma bila kufukuzwa shule kwa  sababu ya karo. Mpango huo uliopewa jina la Elimu Fund unatarajiwa kuwawezesha wanafunzi kutoka familia maskini kuendeleza masomo  bila tashwishi.

Aidha Nassir  amewahakikisha wakaazi wa kaunti ya hiyo kuwa utawala wale utashughulikia tatizo la mrundiko wa  taka kwenye kaunti hiyo akisema kuwa ndani ya siku mia moja za utawala wake wanatarajia kuanza zoezi la kuokota na kuchakata taka hizo ili kusafisha mazingira.

Miongoni mwa viongozi wa kuu wa n mrengo Azimio walijitokeza katika sherehe hiyo ni pamoja na Martha Karua pamoja na Kalonzo Musyoka.

Aug 19, 2022

SABABU ZA RUTO KUIMARIKA PWANI KATIKA UCHAGUZI MKUU

 

 

Licha ya kuwa mgombeaji wa kiti Cha Urais Kupitia  Muungano wa Azimio One Kenya  Raila Odinga amefanikiwa  kwa mara nyengine tena  kuibuka  na kura nyingi katika kanda wa pwani katika uchaguzi mkuu uliyotamatika, rais mteule William Ruto kwa upande wake amefanikiwa kupunguza pengo lilokuwa hapo awali na imani kuwa kuwa kanda ya pwani  ni ngome ya kisiasa ya Bwana Odinga.

Ruto pamoja na timu yake ya Kampeni walitumia mikakati amabayo iliwawezesha kupata  kura takriban laki 336,478 katika kaunti sita za pwani amabzo zinajumuisha  ile ya Mombasa, Lamu, Tana River, Kwale, Kilifi and Taita Taveta. Hesabu hiyo ikiwa ni Ongezeko kutoka Kura hizo ikiwa ni Ongezeko kutoka kura  287,606 ambazo chama cha Jubilee kulifanikiwa kupata katika uchaguzi wa mwaka 2017 ambao uliwapa ushindi rais Uhuru Kenyatta pamoja na Ruto.

Wadadisi wa maswala ya kisiasa wanahoji kuwa Ongezeko la Kura alizozipata Bwana Ruto Katika kanda ya Pwani  zinatokana na hatua yake ya kuwavuta  Viongozi tajika wa eneo hilo upande wake pamoja na kuandaa vikao vya kujadili maswala ya maendeleo eneo hilo ili kuwavutia wapiga kura kujifungamanisha na chama chake cha UDA.

Katika kampeni zake rais Mteule William Ruto alionekana kumshutumu vikali Mpinzani wake mkuu Raila Odinga kwa kuwatenga wafuasi wake wa kanda ya pwani jambo ambalo kulingana na wadadisi wa maswala ya kisisiasa wanasema kuwa  lilichangia pakubwa  kwa chama cha ODM kushindwa katika uchaguzi mdogo eneo bunge la Msambweni amabapo mgombeaji  kutoka chama cha UDA  Faisal Bader aliibika na ushindi.Uchaguzi huo ukiweka msingi kwa Rais Mteule William Ruto kuenziwa nawakaazi wa kanda ya pwani.  

Aug 18, 2022

SARAI AIKOSOA IEBC KUHAIRISHA UCHAGUZI WA UGAVANA

 

Mgombeaji wa kiti cha Ugavana katika kaunti ya Mombasa kupitia kwa chama cha UDA Hassan Omar Sarai ameikosoa tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC kufuatia hatua yake hapo Jana kuahirisha tena uchaguzi wa Ugavana katika kaunti hiyo.

Akizungumza katika kikao na wananahabari mjini Mombasa,Sarai ameitaja hatua hiyo ya IEBC kama inayoongeza hofu miongoni mwa wakaazi wa kaunti hiyo huku akimtaka mwenyekiti wa time hiyo wafula Chebukati kuweka tarehe kamili ambapo uchaguzi huo utaandaliwa.




Wakati huo huo Sarai amewatahadharisha maafisa wa usalama dhidi ya Kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa,akisema kuwa licha ya Maafisa hao kuwahujumu, kamwe hawatalipiza kisasi huku akiwataka kutekeleza majukumu yao kulingana na katiba.


Kwa upande Mgombea mwenza wa Sarai katika kinyang’anyiro hicho Selina Maitha amewatolea wito wakaazi wa Mombasa kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuwapa fursa ya kuongoza kaunti hiyo Ili kuleta mageuzi ya Kimaendeleo.


Mar 10, 2022

SERIKALI KUIMARISHA USALAMA BAHARINI


 

Serikali ya kitaifa imejikita katika kuunda mkakati wa kitaifa wa usalama wa baharini unaonuia kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazotokana na shughuli za uchumi samawati. Mkakati huo utakaohusisha kamati ya kitaifa ya Usalama wa baharini na sajili ya sajili ya kitaifa ya usalama wa baharini, ni mkakati wa kisera utakaojumuisha malengo na ruwaza ya kuimarisha usalama wa majini katika taifa hili .

Akizungumza mjini Mombasa katika  warsha ya ufunguzi wa mkakati huo ,katibu wa kudumu katika idara ya taifa ya maswala ya Afrika Mashariki daktari Kevit Desai,amesema kuwa mkakati huo umeundwa ili kurahisisha  ushirikiano baina ya wadau pamoja na uangalizi wa hatari na vitisho katikia sekta ya shughuli za baharini.

 Aidha Desai amebainisha kuwa uchumi samawati unashikilia nafasi ya nane miongoni mwa mihimili ya kiuchumi katika ruwaza ya mwaka 2030 na ya tatu katika agenda nne kuu za serikali,akisema kuwa taifa hili taifa hili limejiandaa vilivyo katika kutekeleza jukumu muhimu la kuhakikisha usalama katika bahari hindi.

Wakati huo huo amesema kuwa ipo haja ya kulinda usalama wa majini kutokana na vitisho vya ndani na nje ya nchi ili kuruhusu usafirishaji wa watu na mizigo ufanyike kwa njia ya amani kwani  unachangia biashara kwa asilimia tisini katika ukanda huu.

Mar 2, 2022

MOMBASA ILIVYOATHIRIKA NA VITA NCHINI UKRAINE

 Na Nyota  Suleiman.

Mzozo unaoendelea hivi sasa baina ya Mataifa ya Ukraine na Urusi bila shaka  umesababisha  athari ya Moja kwa moja kwa Kaunti ya Mombasa.Mnamo mwaka jana serikali ya Kaunti ya Mombasa iliingia  makubaliano ya ushirika  na upatanisho wa kibiashara baina ya serikali na wadau binafsi katika miji  ya Odes na Kiev katika taifa la Ukraine. 


Utawala wa Gavana wa  kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho Ulituma UJumbe kuelekea nchini  Ukraine Ili  kufanya ziara iliyolenga kujenga uhusiano mwema baina ya kaunti ya Mombasa na taifa hilo la Ukraine.Aidha baada ya ziara hiyo ujumbe kutoka  taifa la Ukraine nao pia  uliwasili katika kaunti ya Mombasa kukagua  sehemu za vivutio vya watalii ambavyo vinapatikana katika kaunti ya  Mombasa na pwani ya Kenya kwa Ujumla.

 Makubaliano hayo ya ushirika yaliifanya kaunti ya Mombasa kuanza kupokea Ndege kadhaa za watalii zilizoidhinishwa  kutoka taifa la Ukraine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi.

Aidha Mapema Mwezi wa Februari Mwaka huu Serikali ya kaunti ya Mombasa iliingia katika mkataba mwengine na taifa hilo la  ambao ungewezesha wataalamu mbalimbali  na madaktari katika kaunti ya Mombasa kupata mafunzo katika taifa hilo la Ughaibuni.Hata hivyo vita vinavyoendelea hivi sasa katika Taifa hilo vimeufanya mpango huo kusimama huku hatima yake bado ikiwa haijulikani.Kulingana na Afisa mkuu wa Afya kaunti ta Mombasa daktari Khadija Shikely kundi la kwanza la madaktari hao lilitarajiwa kusafiri nchini Ukraine mwanzoni mwa mwezi  Machi.

Mbali na Ushirikiano katika sekta ya Matibabu  Taifa la Ukraine limekuwa likishirikiana na Kaunti  ya  Mombasa katika kukuza utalii lakini kutokana na kuzuka kwa vita hatima ya makubaliano hayo ya Ushirika kwa sasa haijulikani  .

Feb 25, 2022

DARAJA LA MAKUPA KUANZA KUTUMIKA JUNI

 NA NYOTA SULEIMAN

Halmashauri ya barabara kuu za Kenya KENHA Imesema kuwa daraja la Makupa  lilogharimu jumla ya shilingi bilioni 4.5 linatarajiwa kuanza  kutumika mwezi  juni mwaka huu.Daraja hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwezi Aprili mwaka jana kwa sasa limekamilika kwa asilimia hamsini na saba.


Aidha Kulinagana na Mhandisi mkaazi wa mradi huo  Stephen Gicheru ni kwamba awali mradi huo ulitarajiwa kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili  lakini kutokana na kucheleshwa kwa kazi muhimu katika ujenzi huo kuliwalazimu kutathmini upya muda wa kuukamilisha .

Gicheru pia ameongezea kuwa ipo mipango ya kuiondoa barabara ya Makupa Courseway baada ya kukamilika kwa daraja hilo lakini hilo huenda likachukua muda zaidi.

Wakati huo huo  amesema kuwa wanatarajia daraja hilo litaanza kutumika punde tu  baada ya kukamilika kwake ,huku kazi nyengine zilizosalia zikiendelezwa huku likitumika  .Kandarasi  ya kulikarabati daraja hilo lenye urefu wa mita 457 ambalo litaunganisha eneo la Tudor na port reitz ilipewa kampuni ya China Construction Coporation mwezi novemba mwaka 2020.

 

Feb 18, 2022

KAMPUNI YA PEPSI YAFUNGUA BOHARI MOMBASA

 





Ushindani katika sekta ya utengenezaji wa vinywaji nchini  unatarajiwa kuongezeka kufuatia hatua ya kampuni maarufu duniani inayojishuguhulisha na utengenezaji  wa vinywaji ya Pepsi kuzindua bohari  katika kaunti ya Mombasa, huku kampuni hiyo ikilenga  kupenyeza  katika soko la ukanda  wa Afrika Mashariki.

Akizungumza  wakati wa kuzinduliwa kwa bohari hilo katika kaunti ya Mombasa  ,Afisa anayelisimamia salim Oganda amesema kuwa kampuni ya Pepsi  kwa miaka mingu imetamani  kupanua wigo wake  katika ukanda wa pwani kutokana na udhabiti wa soko lake eneo hili.

Aidha Ameongezea kuwa kwa sasa kampuni hiyo inalenga  soko la pwani ya Kenya baada ya kufungua maduka katika kaunti za Kisumu na Nairobi akiongezea kuwa  kufikia sasa zaidi ya watu arubaini wameajiriwa na wengine zaidi wakitarajiwa kuajiriwa katika siku za usoni.

Kwa upande wake Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir ambaye alihudhuria uzinduzi huo amewarai wawekezaji kuekeza katika ukanda wa pwani kutokana na ukuaji wa utalii katika eneo hili huku akiitolea wito  serikali kutathmini upya ushuru unaowekewa  wawekezaji wapya wa wakigeni.

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...