NA NYOTA SULEIMAN
Halmashauri ya barabara kuu za Kenya KENHA Imesema kuwa
daraja la Makupa lilogharimu jumla ya
shilingi bilioni 4.5 linatarajiwa kuanza
kutumika mwezi juni mwaka
huu.Daraja hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwezi Aprili mwaka jana kwa sasa
limekamilika kwa asilimia hamsini na saba.
Aidha Kulinagana na Mhandisi mkaazi wa mradi huo Stephen Gicheru ni kwamba awali mradi huo
ulitarajiwa kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili lakini kutokana na kucheleshwa kwa kazi
muhimu katika ujenzi huo kuliwalazimu kutathmini upya muda wa kuukamilisha .
Gicheru pia ameongezea kuwa ipo mipango ya kuiondoa barabara
ya Makupa Courseway baada ya kukamilika kwa daraja hilo lakini hilo huenda
likachukua muda zaidi.
Wakati huo huo
amesema kuwa wanatarajia daraja hilo litaanza kutumika punde tu baada ya kukamilika kwake ,huku kazi nyengine
zilizosalia zikiendelezwa huku likitumika .Kandarasi ya kulikarabati daraja hilo lenye urefu wa
mita 457 ambalo litaunganisha eneo la Tudor na port reitz ilipewa kampuni ya China Construction
Coporation mwezi novemba mwaka 2020.