Ushindani katika sekta ya utengenezaji wa vinywaji nchini unatarajiwa kuongezeka kufuatia hatua ya kampuni maarufu duniani inayojishuguhulisha na utengenezaji wa vinywaji ya Pepsi kuzindua bohari katika kaunti ya Mombasa, huku kampuni hiyo ikilenga kupenyeza katika soko la ukanda wa Afrika Mashariki.
Akizungumza wakati wa kuzinduliwa kwa bohari hilo katika kaunti ya Mombasa ,Afisa anayelisimamia salim Oganda amesema kuwa kampuni ya Pepsi kwa miaka mingu imetamani kupanua wigo wake katika ukanda wa pwani kutokana na udhabiti wa soko lake eneo hili.
Aidha Ameongezea kuwa kwa sasa kampuni hiyo inalenga soko la pwani ya Kenya baada ya kufungua maduka katika kaunti za Kisumu na Nairobi akiongezea kuwa kufikia sasa zaidi ya watu arubaini wameajiriwa na wengine zaidi wakitarajiwa kuajiriwa katika siku za usoni.
Kwa upande wake Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir ambaye alihudhuria uzinduzi huo amewarai wawekezaji kuekeza katika ukanda wa pwani kutokana na ukuaji wa utalii katika eneo hili huku akiitolea wito serikali kutathmini upya ushuru unaowekewa wawekezaji wapya wa wakigeni.