Mar 10, 2022

SERIKALI KUIMARISHA USALAMA BAHARINI


 

Serikali ya kitaifa imejikita katika kuunda mkakati wa kitaifa wa usalama wa baharini unaonuia kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazotokana na shughuli za uchumi samawati. Mkakati huo utakaohusisha kamati ya kitaifa ya Usalama wa baharini na sajili ya sajili ya kitaifa ya usalama wa baharini, ni mkakati wa kisera utakaojumuisha malengo na ruwaza ya kuimarisha usalama wa majini katika taifa hili .

Akizungumza mjini Mombasa katika  warsha ya ufunguzi wa mkakati huo ,katibu wa kudumu katika idara ya taifa ya maswala ya Afrika Mashariki daktari Kevit Desai,amesema kuwa mkakati huo umeundwa ili kurahisisha  ushirikiano baina ya wadau pamoja na uangalizi wa hatari na vitisho katikia sekta ya shughuli za baharini.

 Aidha Desai amebainisha kuwa uchumi samawati unashikilia nafasi ya nane miongoni mwa mihimili ya kiuchumi katika ruwaza ya mwaka 2030 na ya tatu katika agenda nne kuu za serikali,akisema kuwa taifa hili taifa hili limejiandaa vilivyo katika kutekeleza jukumu muhimu la kuhakikisha usalama katika bahari hindi.

Wakati huo huo amesema kuwa ipo haja ya kulinda usalama wa majini kutokana na vitisho vya ndani na nje ya nchi ili kuruhusu usafirishaji wa watu na mizigo ufanyike kwa njia ya amani kwani  unachangia biashara kwa asilimia tisini katika ukanda huu.

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...