Mgombeaji wa kiti cha Ugavana katika kaunti ya
Mombasa kupitia kwa chama cha UDA Hassan Omar Sarai ameikosoa tume huru ya
Uchaguzi na Mipaka nchini IEBC kufuatia hatua yake hapo Jana kuahirisha tena
uchaguzi wa Ugavana katika kaunti hiyo.
Akizungumza katika kikao na wananahabari mjini
Mombasa,Sarai ameitaja hatua hiyo ya IEBC kama inayoongeza hofu miongoni mwa
wakaazi wa kaunti hiyo huku akimtaka mwenyekiti wa time hiyo wafula Chebukati kuweka
tarehe kamili ambapo uchaguzi huo utaandaliwa.
Wakati huo huo Sarai amewatahadharisha maafisa wa
usalama dhidi ya Kutumiwa vibaya na baadhi ya wanasiasa,akisema kuwa licha ya
Maafisa hao kuwahujumu, kamwe hawatalipiza kisasi huku akiwataka kutekeleza
majukumu yao kulingana na katiba.
Kwa upande Mgombea mwenza wa Sarai katika
kinyang’anyiro hicho Selina Maitha amewatolea wito wakaazi wa Mombasa kujitokeza
kwa wingi siku ya kupiga kura na kuwapa fursa ya kuongoza kaunti hiyo Ili kuleta
mageuzi ya Kimaendeleo.
