Licha ya kuwa mgombeaji wa kiti Cha Urais Kupitia Muungano wa Azimio One Kenya Raila Odinga amefanikiwa kwa mara nyengine tena kuibuka na kura nyingi katika kanda wa pwani katika
uchaguzi mkuu uliyotamatika, rais mteule William Ruto kwa upande wake amefanikiwa
kupunguza pengo lilokuwa hapo awali na imani kuwa kuwa kanda ya pwani ni ngome ya kisiasa ya Bwana Odinga.
Ruto pamoja na timu yake ya Kampeni walitumia
mikakati amabayo iliwawezesha kupata kura takriban laki 336,478 katika kaunti sita za
pwani amabzo zinajumuisha ile ya Mombasa,
Lamu, Tana River, Kwale, Kilifi and Taita Taveta. Hesabu hiyo ikiwa ni Ongezeko
kutoka Kura hizo ikiwa ni Ongezeko kutoka kura 287,606 ambazo chama cha Jubilee kulifanikiwa
kupata katika uchaguzi wa mwaka 2017 ambao uliwapa ushindi rais Uhuru Kenyatta
pamoja na Ruto.
Wadadisi
wa maswala ya kisiasa wanahoji kuwa Ongezeko la Kura alizozipata Bwana Ruto
Katika kanda ya Pwani zinatokana na hatua
yake ya kuwavuta Viongozi tajika wa eneo
hilo upande wake pamoja na kuandaa vikao vya kujadili maswala ya maendeleo eneo
hilo ili kuwavutia wapiga kura kujifungamanisha na chama chake cha UDA.
