Rais wa Burundi Evariste Ndayishimiye anatarajiwa kuwasili humu nchini siku ya jumatatu na anatarajiwa kuhudhuria sherehe za mwaka huu za Madaraka siku ya jumanne kama mgeni wa heshima.
msemaji wa Ikulu Kanze Dena amesema kuwa Rais Evariste Ndayishimiye atawasili katika mji wa Kisumu siku ya jumatatu ili kuanza ziara yake rasmi ya siku mbili nchini.
Rais Ndayishimiye, ambaye ataandamana na mama wa taifa wa jamhuri ya taifa la Burundi, bi Angeline Ndayubaha, ataungana na rais Uhuru Kenyatta katika ziara ya miradi mbalimbali ya kitaifa katika na kaunti ya Kisumu na eneo la Nyanza kwa ujumla.
Katika ziara hiyo ya siku mbili mama wa taifa wa Kenya bi Margaret Kenyatta na mwezake wa Burundi Angeline Ndayubaha watajihusisha na mazungumzo mbalimbali.