Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano Francis Ole Kaparo amewarai viongozi kutoka jamii za wafugaji kutafuta njia za kusuluhisha migogori iliyodumu kwa muda mrefu baina yao.
Kaparo aliyaongea hayo alipokutana na viongozi kutoka jamii zinazozozana mara kwa mara za pokot na Samburu.Aliwasihi viongozi wa jamii hizo kutafuta suluhisho la kudumu ambalo litasaidia kumaliza mashambulizi ya kulipiza kisasi na wizi wa mifugo miongoni mwao.
Aidha mwenyekiti huyo wa zamani wa NCIC alionyesha kusikitishwa kwake na jamii hizo mbili ambazo zimekuwa zikijuhusisha na mashambulizi ya kulipiza kisasi yanayosababisha wizi wa mifugo.
Vile vile aliwashtumu baadhi ya viongozi wa jamii za wafugaji na wasomi kutoka kaunti za Laikipi, Samburu,Isiolo na Baringo kwa kushindwa kumaliza migogoro hiyo inayoendelea kuongezeka na ambayo imesababisha vifo katika jamii.