May 31, 2021

PICHA ZA KUWASILI KWA RAIS EVARISTE NDAYISHIMIYE WA BURUNDI NCHINI.

KAFYU YAONGEZWA SIKU SITINI ZAIDI

Marufuku ya kitaifa ya watu kutotoka nje kuanzia saa nne usiku hadi saa kumi alfajiri imeongezwa kwa siku sitini zaidi.
 
Kupitia notisi ya sheria nambari 89, Waziri wa usalama wa ndani Fred Matiang'i amesema kuwa agizo hilo litatekelezwa katika maeneo yote ya jamhuri ya taifa la Kenya.

Agizo hilo lilianza kutekelezwa tarehe 28 Mei 2021 na litaendelea kwa kipindi cha siku sitini.
 
Serikali aidha imekataza mikusanyiko ya umma , matembezi ya mtu mmoja mmoja au makundi nyakati za kafyu, isipokuwa kwa idhini kupitia njia ya maandishi , itakayotolewa na afisa wa polisi anayehudumu katika kaunti au eneobunge. 

May 30, 2021

JAMII ZA WAFUGAJI ZATAKIWA KUKOMESHA VITA

Aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya uwiano na utangamano Francis Ole Kaparo amewarai viongozi kutoka jamii za wafugaji kutafuta njia za kusuluhisha migogori iliyodumu kwa muda mrefu baina yao. 

Kaparo aliyaongea hayo alipokutana na viongozi kutoka jamii zinazozozana mara kwa mara za pokot na Samburu.Aliwasihi viongozi wa jamii hizo kutafuta suluhisho la kudumu ambalo litasaidia kumaliza mashambulizi ya kulipiza kisasi na wizi wa mifugo miongoni mwao. 

Aidha mwenyekiti huyo wa zamani wa NCIC alionyesha kusikitishwa kwake na jamii hizo mbili ambazo zimekuwa zikijuhusisha na mashambulizi ya kulipiza kisasi yanayosababisha wizi wa mifugo. 


Vile vile aliwashtumu baadhi ya viongozi wa jamii za wafugaji na wasomi kutoka kaunti za Laikipi, Samburu,Isiolo na Baringo kwa kushindwa kumaliza migogoro hiyo inayoendelea kuongezeka na ambayo imesababisha vifo katika jamii. 


May 29, 2021

RAIS WA BURUNDI KUZURU KENYA

Rais wa  Burundi Evariste Ndayishimiye anatarajiwa kuwasili humu nchini siku ya jumatatu na anatarajiwa kuhudhuria sherehe za mwaka huu za Madaraka siku ya jumanne kama mgeni wa heshima.
msemaji wa Ikulu Kanze Dena amesema kuwa  Rais Evariste Ndayishimiye atawasili katika mji wa Kisumu siku ya jumatatu ili kuanza ziara yake rasmi ya siku mbili  nchini.

Rais Ndayishimiye, ambaye ataandamana na mama wa taifa wa jamhuri ya taifa la Burundi, bi  Angeline Ndayubaha, ataungana na rais Uhuru Kenyatta katika ziara ya miradi mbalimbali ya kitaifa katika na kaunti ya Kisumu na eneo la Nyanza kwa ujumla. 

Katika ziara hiyo ya siku mbili mama wa taifa wa Kenya bi Margaret Kenyatta na mwezake wa Burundi Angeline Ndayubaha watajihusisha na mazungumzo mbalimbali. 


WAHALIFU WAKAMATWA KIAMBU

Makachero kutoka idara ya upelekezi ya DCI siku ya Ijumaa walimkamata Irene Njoki Irungu kwa madai ya kuwalaghai wateja katika kumbi za starehe kwa kuwawekea  dawa katika vinywaji vyao katika Kaunti ya Kiambu na vitongoji vyake. 
Kulingana na ripoti ya polisi iliyotolewa muda mfupi baada ya kukamatwa kwake na kuzuiliwa,  Mshukiwa alijibandika jina la Mitchelle ili kulinda utambulisho wake. 
Katika kile kilichogundulika na makachero wa DCI kama uwepo wa mzunguko wa genge la wahalifu  linaloendesha biashara hiyo, Mshukiwa na msaidizi wake Peter Irungu,  ambaye pia yuko mikononi mwa polisi, wanashirikiana kunyemelea wateja na kuwawekea dawa katika vinywaji vyao na baadaye kuwaibia. 
Kulingana na Makachero , dawa wanayoitumia kuwalaghai wateja huwafanya waathiriwa kupoteza fahamu kwa zaidi ya saa kumi na mbili,  jambo linalowapa fursa kutekeleza wizi wao na kutoroka bila ya kukamatwa. 
Wakati wa kukamatwa kwake polisi walifanikiwa kunasa simu na laini kadhaa zinazoaminika kuwa ni za waathiriwa wa ulaghai huo. 

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...