Feb 25, 2022

DARAJA LA MAKUPA KUANZA KUTUMIKA JUNI

 NA NYOTA SULEIMAN

Halmashauri ya barabara kuu za Kenya KENHA Imesema kuwa daraja la Makupa  lilogharimu jumla ya shilingi bilioni 4.5 linatarajiwa kuanza  kutumika mwezi  juni mwaka huu.Daraja hilo ambalo ujenzi wake ulianza mwezi Aprili mwaka jana kwa sasa limekamilika kwa asilimia hamsini na saba.


Aidha Kulinagana na Mhandisi mkaazi wa mradi huo  Stephen Gicheru ni kwamba awali mradi huo ulitarajiwa kukamilika ndani ya miezi kumi na mbili  lakini kutokana na kucheleshwa kwa kazi muhimu katika ujenzi huo kuliwalazimu kutathmini upya muda wa kuukamilisha .

Gicheru pia ameongezea kuwa ipo mipango ya kuiondoa barabara ya Makupa Courseway baada ya kukamilika kwa daraja hilo lakini hilo huenda likachukua muda zaidi.

Wakati huo huo  amesema kuwa wanatarajia daraja hilo litaanza kutumika punde tu  baada ya kukamilika kwake ,huku kazi nyengine zilizosalia zikiendelezwa huku likitumika  .Kandarasi  ya kulikarabati daraja hilo lenye urefu wa mita 457 ambalo litaunganisha eneo la Tudor na port reitz ilipewa kampuni ya China Construction Coporation mwezi novemba mwaka 2020.

 

Feb 18, 2022

KAMPUNI YA PEPSI YAFUNGUA BOHARI MOMBASA

 





Ushindani katika sekta ya utengenezaji wa vinywaji nchini  unatarajiwa kuongezeka kufuatia hatua ya kampuni maarufu duniani inayojishuguhulisha na utengenezaji  wa vinywaji ya Pepsi kuzindua bohari  katika kaunti ya Mombasa, huku kampuni hiyo ikilenga  kupenyeza  katika soko la ukanda  wa Afrika Mashariki.

Akizungumza  wakati wa kuzinduliwa kwa bohari hilo katika kaunti ya Mombasa  ,Afisa anayelisimamia salim Oganda amesema kuwa kampuni ya Pepsi  kwa miaka mingu imetamani  kupanua wigo wake  katika ukanda wa pwani kutokana na udhabiti wa soko lake eneo hili.

Aidha Ameongezea kuwa kwa sasa kampuni hiyo inalenga  soko la pwani ya Kenya baada ya kufungua maduka katika kaunti za Kisumu na Nairobi akiongezea kuwa  kufikia sasa zaidi ya watu arubaini wameajiriwa na wengine zaidi wakitarajiwa kuajiriwa katika siku za usoni.

Kwa upande wake Mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir ambaye alihudhuria uzinduzi huo amewarai wawekezaji kuekeza katika ukanda wa pwani kutokana na ukuaji wa utalii katika eneo hili huku akiitolea wito  serikali kutathmini upya ushuru unaowekewa  wawekezaji wapya wa wakigeni.

Feb 9, 2022

The Predicarment of Campus Toxic Relationships


 

Reports concerning cases of toxic or unhealthy relationships among Campus students in the Country have been rampant in the current years .While many many people establish relationships and find love in the institutions of higher learning ,Campus relationships  are the main cause of of this unfortunate predicarment.Toxic or unhealthy relationship can be defined as a relationship where one partner control aspects of the other partner's life and can be abusive in apsychological ,physical or sexual way.The person getting abused can be described as the victim .

Consequently There are several factors which influence toxic relationships among campus intimate partners among them lack of trust ,Infidelity and alcohol and drug abuse among others.As a consequence of being in a toxic relationship many students both male and female find themselves with serious injuries ,disability or sometimes even loosing their lives.At the same time many Victims of campus  toxic relationships often suffer from low self esteem and poor academic performance simply because they are unable to put their concentration in their studies.

Given these effects one may questions why anyone would remain in these campus toxic relationships .One reason people stay in an unhealthy or toxic relationship is because they do not think they will get justice from their partners.Another reason is because the victim always know their abusers well and  is reluctant to report this person and get this person in trouble .

In conclusion Toxic Campus relationships among Students is very prevalent.The main Factors that influence partners to be toxic are mainly infidelity,mistrusts, and alcohol and drug abuse.Although there are structures in place that can help survivors of these kind of  relationships There needs to be effective and clear laws that hinder toxic relationships among students in the institutions of higher learning.

REFFERENCE 

1. Arnett, J.J. (2000). Emerging adulthood: A theory of development from the late teens through the twenties. American Psychologist, 55, 469-480.

2.Nation Africa,  28 JUN 2020 https://nation.africa/kenya/news/what-pushes-college-students-to-commit-suicide--152908?view=htmlamp

Feb 2, 2022

WAKAAZI WA CHANGAMWE WATAKIWA KUJISAJILI NA IEBC SAWIA NA CHAMA CHA ODM

 


NA NYOTA SULEIMAN MOHAMED

Viongozi mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kuwahimiza wananchi kujiandikisha kama wapiga kura kabla la zoezi kufungwa.

katika kaunti ya Mombasa Uongozi wa chama cha ODM  umefanya misururu ya mikutano katika eneo bunge la Changamwe ili kuwahamasisha wananchi   kujitokeza kwa wingi  na kujisajili kama wapiga kura pamoja kujiandikisha kuwa wanachama wa chama hicho.


 

Akiongoza msafara huo Mwenyekiti wa Chama cha ODM kaunti ya Mombasa Mohamed Khamid Khamis maarufu DEE amewarai wananchi katika eneo bunge hilo kujisajili kwa wingi  kama wapiga kura ili kumpeleka Ikulu  kinara wa Chama hicho Raila Odinga baada ya uchaguzi mkuu.


Aidha Mohamed ameendelea kusisitiza kuwa uteuzi wa chama hicho utafanyika kwa njia huru na haki,akiwahimiza wakaazi wa Changamwe kuchukua kura kwa wingi na kusajili katika chama cha  ODM , akisema kuwa ni  wale waliojisajili na chama pekee ndio watakao ruhusiwa kupiga kura katika kura za mchujo.

Kwa Upande wake katibu mkuu wa chama cha ODM kaunti ya Mombasa Geoffrey Busaka ameendelea kumpigia debe kinara wa chama hicho Raila Odinga akisema kwamba juhudi za kinara wa chama cha ODM Raila Odinga za kuingia ikulu zitategemea mno na kura za Wakaazi wa Kaunti nzima ya Mombasa.

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...