Mar 10, 2022

SERIKALI KUIMARISHA USALAMA BAHARINI


 

Serikali ya kitaifa imejikita katika kuunda mkakati wa kitaifa wa usalama wa baharini unaonuia kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazotokana na shughuli za uchumi samawati. Mkakati huo utakaohusisha kamati ya kitaifa ya Usalama wa baharini na sajili ya sajili ya kitaifa ya usalama wa baharini, ni mkakati wa kisera utakaojumuisha malengo na ruwaza ya kuimarisha usalama wa majini katika taifa hili .

Akizungumza mjini Mombasa katika  warsha ya ufunguzi wa mkakati huo ,katibu wa kudumu katika idara ya taifa ya maswala ya Afrika Mashariki daktari Kevit Desai,amesema kuwa mkakati huo umeundwa ili kurahisisha  ushirikiano baina ya wadau pamoja na uangalizi wa hatari na vitisho katikia sekta ya shughuli za baharini.

 Aidha Desai amebainisha kuwa uchumi samawati unashikilia nafasi ya nane miongoni mwa mihimili ya kiuchumi katika ruwaza ya mwaka 2030 na ya tatu katika agenda nne kuu za serikali,akisema kuwa taifa hili taifa hili limejiandaa vilivyo katika kutekeleza jukumu muhimu la kuhakikisha usalama katika bahari hindi.

Wakati huo huo amesema kuwa ipo haja ya kulinda usalama wa majini kutokana na vitisho vya ndani na nje ya nchi ili kuruhusu usafirishaji wa watu na mizigo ufanyike kwa njia ya amani kwani  unachangia biashara kwa asilimia tisini katika ukanda huu.

Mar 2, 2022

MOMBASA ILIVYOATHIRIKA NA VITA NCHINI UKRAINE

 Na Nyota  Suleiman.

Mzozo unaoendelea hivi sasa baina ya Mataifa ya Ukraine na Urusi bila shaka  umesababisha  athari ya Moja kwa moja kwa Kaunti ya Mombasa.Mnamo mwaka jana serikali ya Kaunti ya Mombasa iliingia  makubaliano ya ushirika  na upatanisho wa kibiashara baina ya serikali na wadau binafsi katika miji  ya Odes na Kiev katika taifa la Ukraine. 


Utawala wa Gavana wa  kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho Ulituma UJumbe kuelekea nchini  Ukraine Ili  kufanya ziara iliyolenga kujenga uhusiano mwema baina ya kaunti ya Mombasa na taifa hilo la Ukraine.Aidha baada ya ziara hiyo ujumbe kutoka  taifa la Ukraine nao pia  uliwasili katika kaunti ya Mombasa kukagua  sehemu za vivutio vya watalii ambavyo vinapatikana katika kaunti ya  Mombasa na pwani ya Kenya kwa Ujumla.

 Makubaliano hayo ya ushirika yaliifanya kaunti ya Mombasa kuanza kupokea Ndege kadhaa za watalii zilizoidhinishwa  kutoka taifa la Ukraine katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Moi.

Aidha Mapema Mwezi wa Februari Mwaka huu Serikali ya kaunti ya Mombasa iliingia katika mkataba mwengine na taifa hilo la  ambao ungewezesha wataalamu mbalimbali  na madaktari katika kaunti ya Mombasa kupata mafunzo katika taifa hilo la Ughaibuni.Hata hivyo vita vinavyoendelea hivi sasa katika Taifa hilo vimeufanya mpango huo kusimama huku hatima yake bado ikiwa haijulikani.Kulingana na Afisa mkuu wa Afya kaunti ta Mombasa daktari Khadija Shikely kundi la kwanza la madaktari hao lilitarajiwa kusafiri nchini Ukraine mwanzoni mwa mwezi  Machi.

Mbali na Ushirikiano katika sekta ya Matibabu  Taifa la Ukraine limekuwa likishirikiana na Kaunti  ya  Mombasa katika kukuza utalii lakini kutokana na kuzuka kwa vita hatima ya makubaliano hayo ya Ushirika kwa sasa haijulikani  .

HIVI PUNDE

Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa

Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa  mbunge wa EALA...