Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai na wale wa Mbunge wa Nyali Mohammed Ali kuonyeshana ubabe wa kisiasa.
Jun 24, 2023
Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa
Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa mbunge wa EALA Hassan Omar Sarai na wale wa Mbunge wa Nyali Mohammed Ali kuonyeshana ubabe wa kisiasa.
AFUENI KWA MADEREVA WA TUK TUK MOMBASA
Na Nyota Suleiman
MADEREVA wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kampuni ya Car General Kuzindua rasmi aina mpya za Tuk Tuk PIAGGIO NXT zenye Muundo wa kipee ambazo zinatarajiwa kupiga Jeki biashara hiyo na kuiboresha zaidi katika kaunti hiyo.
Uzinduzi wa aina hiyo mpya ya Tuk Tuk unajiri kufuatia malalamiko kutoka kwa madereva wa Tuk Tuk kuhusiana na mapungufu yaliyoshuhudiwa katika Tuk Tuk za hapo awali zilizonunuliwa kutoka kwa kampuni hiyo.
Kulingana na raisi wa Muunganao wa madereva wa Tuk Tuk kaunti ya Mombasa ambaye pia ni mwanzilishi wa biashara hiyo katika kaunti hiyo Chrispine Obondo maarufu Mr Dubai ameutaja uzinduzi huo kama hatua muhimu katika sekta ya uchukuzi katika kaunti ya Mombasa akisema itawasaidia pakubwa madereva wa Tuk Tuk kumudu gharama ya biashara hususan bei ya mafuta kutokana na muundo wa Kipekee wa Tuk Tuk Hizo.
Wakati huo huo ameipongeza kampuni ya Car and general kwa kutoa kipaumbele katika kuangazia maslahi na matatizo yanayowakumba Madereva na kutafuta suluhu muafaka ili Kuwawezesha kuendeleza biashara bila madhila yoyote.
Aidha ametoa wito kwa madereva wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa kupewa mafunzo ya Kutosha kuwawezesha kuendeleza shughuli zao ipasavyo ili kuwaepushia mahangaiko wanayopitia kutoka kwa maafisa trafiki katika kaunti hiyo.
Wakati huo huo ameonyesha kusikitishwa kwake na jinsi baadhi ya maafisa hao wa trafiki wamekuwa wakiwahanagaisha madereva wa tuk tuk bila hatia ,akiwataka kukomesha hujuma dhidi yao.
Baadhi ya Madereva waliyozungumza katika hafla ya Uzinduzi huo iliyoandaliwa katika uga wa Makadara mjini Mombasa Wameonyesha furaha yao kutokana ujio wa Tuk Tuk hizo mpya huku wakiwarai wenzao kujiunga na miungano ya madereva ili wawaze kujinufaisha zaidi.
Kwa upande wao maafisa kutoka kampuni ya Car and general waliyohudhuria uzinduzi huo wamewahimiza madereva kujitokeza na kuchukua mikopo ya kununua Tuk Tuk hizo mpya ili waweze kujiendeleza zaidi kichumi.
HIVI PUNDE
Ghasia zatanda kwenye mkutano wa UDA Mombasa
Hali purukushani imeshuhudiwa Leo wakati wa mkutano wa wajumbe wa Chama Cha UDA kwenye kaunti ya Mombasa baada ya wafuasi wa mbunge wa EALA...
-
NA NYOTA SULEIMAN MOHAMED Viongozi mbalimbali wamekuwa mstari wa mbele kuwahimiza wananchi kujiandikisha kama wapiga kura kabla la zoezi k...
-
Aliyekuwa Mwaniaji wa Kiti cha ugavana kaunti ya Mombasa Suleiman Shahbal amekihama chama cha Jubilee na kuregea katika chama Cha ODM huku u...
-
Na Nyota Suleiman MADEREVA wa Tuk Tuk katika kaunti ya Mombasa wana kila sababu ya kutabasamu baada ya kampuni ya Car General Kuzindua rasm...


